Hali ya sintofahamu imeibuka jijini Arusha baada ya mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika amedaiwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa kushindwa kurejesha pesa ya vikoba.
Moja ya mwanakikundi mwenzake amesema kuwa marehemu alifika kwenye eneo lake la biashara kwani yeye anauza vichwa vya kuku na kumlalamikia kuwa hana pesa ya marejesho na hajui wapi ataipata.
Mwanakikundi huyo anaendelea kuiambia Global Tv kuwa alimtia moyo marehemu na kumueleza kuwa kufikia jioni watakuwa wameshapata pesa ya kurejesha, lakini cha kushangaza ameitwa na kukuta rafiki yake tayari amejinyonga, na kufariki Dunia.