Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanahabari akutwa amefariki chumbani

93325 Pic+habari Mwanahabari akutwa amefariki chumbani

Tue, 28 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwandishi wa habari Deogratius David amekutwa amekufa chumbani kwake Buguruni jijini Dar es Salaam baada ya kutoonekana kwa siku kadhaa.

Mwili wake umekutwa katika chumba hicho leo Jumatatu Januari 27, 2020 baada ya majirani kuanza kusikia harufu kali.

Mwananchi lilifika eneo hilo na kuzungumza na majirani waliosimulia jinsi polisi walivyofika na kuuchukua mwili wa mwandishi huyo wa habari.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu taarifa za kifo hicho kamanda wa polisi Wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela amesema hana taarifa zozote.

Kwa sharti la kutotajwa jina mmoja wa majirani amesema, “Deo hajaonekana  kwa siku kadhaa na kwenye simu hapatikani lakini kilichotupa wasiwasi ni harufu kali iliyokuwa inatoka kwenye chumba chake.”

“Asubuhi ya leo tukavunja mlango ndio alipokutwa akiwa kitandani kwake mwili ukiwa umeharibika vibaya, hilo ndilo linaloweza kusema kwa kifupi mengine watakuwa nayo polisi.”

Pia Soma

Advertisement
Habari zaidi zinaeleza majirani walitoa taarifa polisi waliofika  eneo hilo na kuchukua mwili wa mwandishi huyo.

Fuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz