Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa kidato cha tatu ajifungua na kutupa mtoto

2c522398c2ff8b3ed80330fa170610c8 Mwanafunzi wa kidato cha tatu ajifungua na kutupa mtoto

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Geita, limethibitisha kupokea taarifa ya kuokotwa kwa kichanga cha siku moja jinsia ya kiume kilichotupwa maeneo ya shule ya msingi Igalula.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kamanda wa polisi Mkoa wa Geita ,Henry Mwaibambe, amesema tukio hilo limetoa Agasti 27,2021 muda wa saa moja usiku

Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo amefahamika na anaitwa Keflini Charles (17) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Kachwamba Wilayani chato.

Mtoto huyo aliokotwa na wananchi na kupelekwa hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri huku mama wa mtoto akijisalimisha na kukabidhiwa mwanae.

Lakini katika tukio lingine tarehe 31/08/2021 saa 3:15 Usiku katika Maeneo ya Mwatulole kata ya buhalahala Mkoa wa Geita ,uliokotwa mwili wa mtoto Jinsia ya kiume mwenye miezi 8 ukiwa umefungwa kwenye mfuko na kutupwa jalalani .

Aidha mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa ajili ya uchunguzi na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi

Chanzo: www.habarileo.co.tz