Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa darasa la saba amwandikia Jokate barua

11360 BARUA+PIC TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amejibu barua ya mwanafunzi Mwanahamisi Yusufu wa darasa la Saba wa Shule ya msingi ya Chanzige B, Kisarawe ya kumtaka aitembelee shule yao.

Jokate ameandika katika ukurasa wake wa twitter leo Agosti 11 na kusema kuwa mwanafunzi huyo alimuandikia barua na akaipokea Jumanne, Agosti 7.

“Aliniomba nitembelee shule yake niongee na wanafunzi wenzake wa darasa la 7. Niliitikia wito jana nikaenda kuwasikiliza,” amesema

 Jokate aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Julai 28 mwaka huu. Kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya, Jokate amewahi kushiriki mashindano ya ulimbwende ya ‘Miss Tanzania’  na kushika namba mbili.

Chanzo: mwananchi.co.tz