Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi mwingine auawa Geita, atobolewa jicho!

Mwai Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe

Tue, 21 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polishi Mkoa wa Geita limesema linaendelea kuchunguza tukio la mauaji ya mtoto (14) Johnson Thomas Mwanafunzi wa Darasa la Saba shule ya Msingi Buhalahala ambaye mwili wake ulikutwa pembeni ya mto Mita 120 kutoka barabara inayotoka Buhalahala senta kuelekea Kijiji cha Nyakato Mjini Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo alitoka nyumbani kwao kwa kutumia Bajaj iliyokuwa inaendeshwa na Benson Theophili Juni 12,2022 majira ya saa 11 jioni.

Ameeleza kuwa mtoto huyo alikuwa alikuwa anaelekea senta kushona sare zake za shule na mara ya mwisho alionekana na Mwanafunzi mwenzake (jina limehifadhiwa)akielekea barabara ya zilipo ofisi za Kampuni ya GPH.

Mwaibambe ameeleza kuwa mtoto huyo hakuonekana tena mpaka alipokutwa amefariki Juni 18,2022 na eneo la tukio linaonyesha mwili huo uliletwa hapo.

Amefafanua kuwa mwili wa marehemu baada ya uchunguzi ulibainika kuwa na majeraha mguu wa kushoto ukiwa umepondwa na kitu kizito na jicho kuumizwa na kugeukia ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live