Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi auawa na mamba akioga Ziwa Victoria

79864 Mamba+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Buchosa. Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Itabagumba Wilayani Sengerema  Mkoa wa Mwanza Tanzania, Magesa Beseko (12) amekufa baada ya kuliwa na mamba alipokuwa akioga ziwani.

Tukio limetokea Oktoba 11, 2019 saa 12 jioni katika Kitongoji cha Msuswiga kilichopo katika kijiji cha Bulyaheke B  Wilayani Sengerema.

Mwanafunzi huyo alienda eneo hilo kwa lengo la kumwagilia bustani ya nyanya inayomilikiwa na baba yake na alipomaliza shughuli hiyo, akaamua kwenda kuoga ziwani.

Baba wa mtoto huyo,  Biseko Kapunda aliliambia Mwananchi kuwa maiti ya mwanawe bado haijapatikana.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji Cha Bulyaheke B,  Barenadetha  Sandu alilithibitishia Mwananchi kutokea kwa kifo hicho na amesema hadi sasa mabaki ya mwili wa mwanafunzi huyo hayajapatikana na wakazi wa eneo hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wanaendelea kutafuta.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Itabagumba Maimuna Hamis amesema kuwa mwanafunzi aliyekubwa na mauti yao anasoma katika shule hiyo Darasa ya sita na amepokea kwa masikitiko juu ya tukio hilo.

Pia Soma

Advertisement
Baba wa mwanafunzi huyo, Biseko Kapunda amesema mwanawe alitoka shuleni akiwa na wenzake na ni kawaida yake kupitia kwenye bustani hiyo kumwagilia na si kawaida yake kuoga ziwani.

“Kila siku jioni alikuwa anaenda kumwagilia bustani yangu ya nyanya na huwa haogi ziwani, cha kushangaza siku ya tukio hilo alikwenda kuoga ziwani akiwa na wenzake na ndipo alikumbwa na mauti hayo,” alisema baba huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alisema hajapata taarifa yoyote juu ya tukio hilo na kuahidi kufuatilia.

Hata hivyo, Kipole amesema matukio ya ya watu kakamatwa na mamba hutokea mara nyingi na hatua iliyochukuliwa hadi sasa ni ya kuwazuia watu wasioge katika ufukwe wa ziwa hilo ili kuepuka madhara kama hayo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz