Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi auawa kwa kuchomwa kisu hosteli Morogoro

Kisu.jpeg Mwanafunzi auawa kwa kuchomwa kisu hosteli Morogoro

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Manispaa ya Morogoro, Hajrat Shaban ameuawa baada ya kuvamiwa akiwa kwenye hosteli za chuo na kuchomwa kisu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama leo Jumatano Aprili 17, 202.

Kamanda Mkama amesema tukio hilo limetokea eneo la Mkundi jana Aprili 16, 2024 ambapo marehemu alichomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo.

“Tunafanya uchunguzi wa kifo cha Hajrat Shaban (22) mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Mtaa wa Bwawani Kata ya Mkundi, tukio hilo lililotokea Aprili 16, 2024 majira ya saa 2:00 usiku.

“Tukio limetokea wakati binti huyo na wenzake wakiwa katika makazi yao ya pamoja (hosteli) ambapo walimkamata kijana mmoja aliyekuwa amekwapua simu, walipojaribu kumdhibiti ndipo alimjeruhi marehemu kwa kumchoma na kisu.

Kabla ya hapo alipelekwa Zahanati iitwayo Habemes ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu,”amesema Kamanda Mkama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live