Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi atoroka nyumbani kisa kufeli darasani

Mwanafunzi Atoroka Mwanafunzi atoroka nyumbani kisa kufeli darasani

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: IPP Media

Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Migombani, Dorice Venance (16), anadaiwa kutoroka nyumbani kwao Tabata Segerea tangu Juni 4, mwaka huu kwa madai ya kufanya vibaya kwenye masomo yake.

Baba mkubwa wa mwanafunzi huyo, Charles Kenyela, aliyefika katika ofisi za Nipashe, zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, alisema Dorice aliondoka nyumbani siku hiyo saa tano usiku, akiwa amevaa shati la rangi ya kahawia na suruali ya kulalia ya bluu.

Alisema alimtoa nyumbani kwao Mwanza baada ya kumaliza elimu ya msingi na kumhamishia Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari ili kumpa msaada wa kielimu.

“Hivi karibuni alishawahi kuniambia kuwa anaomba nimrudishe nyumbani kwao Mwanza kwa sababu anahisi kuwa anapoteza muda kutokana na kufeli mitihani yake kadiri siku zinavyokwenda,” alisema.

Hata hivyo, alisema alimtia moyo na kumshauri aongeze bidii kwa sababu elimu ya kijijini aliposoma msingi ni tofauti na mjini, lakini Jumatano ya wiki iliyopita mtoto huyo alitoroka usiku.

“Tuligundua kuwa ametoroka baada ya kukuta funguo zikining’inia mlangoni na tulipotazama kwenye kamera za CCTV tukamuona alivyokuwa anatoka. Mpaka sasa inakaribia wiki nyumbani kwao Mwanza hajafika na wala hapa nyumbani hayupo,” alisema.

Alisema ameshatoa taarifa Kituo cha Polisi cha Tabata na kupewa RB Na. TBT/RB/2635/2022 kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa kwenye kituo hicho au kupiga simu namba 0754485911 au 0743608494.

Chanzo: IPP Media