Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi apoteza kiganja kwa kuliwa na fisi

Deus Mtoto Mwanafunzi apoteza kiganja kwa kuliwa na fisi

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanafunzi wa Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Kasomeko iliyopo Kata ya Katunguru, Deus Dalama (8) mkazi wa Wilayani Sengerema amejeruhiwa na fisi sehemu mbalimbali za mwili ambapo madhara makubwa aliyoyapata ni mnyama huyo kuondoka na mkono wa Deus.

Tukio limetokea Agosti 2, 2023 wakati Deus alipokuwa akicheza na wenzake ambapo fisi huyo aliwavamia.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo ya Sengerema Senyi Ngaga amewataka Wananchi hao kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama wakali.

Naye, Sadick Jimola ambaye ni Diwani wa Kata ya Katunguru ameiomba Serikali kumpa fidia mtoto Deus kwa kupoteza sehemu ya mkono.

Upande wa Mhifadhi wa Wanyamapori Mkoa wa Mwanza, Godfrey Baisi amesema tayari wametuma kikosi kazi kwenda katika kata husika kwa lengo la kuwaangamiza fisi hao.

Chanzo: Mwanaspoti