Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi aliwa na mamba akioga Ziwa Victoria

Mamba Ziwani.jpeg Mwanafunzi aliwa na mamba akioga Ziwa Victoria

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Maisome iliyoko kata ya Maisome wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza, Mashauri Minani (17) aliyekuwa anasoma amefariki dunia baada ya kuliwa na namba akioga Ziwa Victoria

Akizungumzia tukio hilo ofisa mtendaji kata ya Maisome, Revocatis Michele amethibitisha kutoka kwa tukio na mwili wa mwanafunzi huyo bado haujapatikana huku wakiendelea kuutafuta.

Amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 28 mwaka huu jioni baada ya kutoka shule alikwenda kuoga ziwa Victoria ndipo alipokumbana na dhahama ya kuliwa na mamba.

Matukio ya watu kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba na wengine kujeruhiwa yamekithiri kwa wakazi wanaoishi maeneo ya kandokando mwa Ziwa Victoria.

Mmoja wa wakazi wa kisiwa cha Maisome, Tulubuza Amoni amesema jitihada za haraka zinatakiwa kusambaza maji ya bomba kwenye kisiwa hicho ili kuwaondolea adha wananchi kwenda kuoga ziwa Victoria na kujiepusha kuliwa na wanyama wakali aina ya mamba.

Mkuu wa shule ya Sekondari Maisome, Joseph Magadula amekiru kuwa mwanafunzi huyo aliyeliwa na mamba anatoka katika shule hiyo akisema kuwa tukio hilo limeleta simanzi shuleni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live