Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi ajeruhiwa kwa kuchomwa kisu kisa 4000

Kisuu Mwanafunzi ajeruhiwa kwa kuchomwa kisu kisa 4000

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Mwanafunzi Jackson Stephen wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kagemu iliyoko katika manispaa ya Bukoba, amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera, baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa kisu mara mbili katika paja lake la mguu wa kulia na mwanafunzi mwenzie akidaiwa 4000.

Akizungumza katika wodi namba moja alikolazwa akiendelea na matibabu, mwanafunzi huyo amesema kuwa alikopeshwa shilingi 3,000 na mwenzake na kumtaka alipe shilingi 4,000 ikiwamo shilingi 1,000 ya riba, fedha ambazo alikuwa hajazipata, na kwamba jana wakiwa katika sherehe ya kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Bukoba, alimtaka kulipa deni hilo na aliposhindwa kulipa alimchoma kwa kisu.

"Jana nikiwa kwenye sherehe pale Bukoba sekondari, akaja na marafiki zake akaniona akaniambia nataka hela yangu, nikamwambia si umeishachukua sendo zangu na umeishaziharibu, akaniambia sitaki kukuona kwenye haya maeneo nikamwambia unanifukuza hapa kama nani, akataka kunipiga wakamzuia, mi ndo nikawa nawaambia marafiki zangu walioniuliza kitu gani nilimfanyia, kulikuwa na muuza maembe pembeni akachomoa kisu akanichoma mara mbili nikaanguka chini nikapoteza fahamu" amesema Jackson.

Kwa upande wake Daktari Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Emmanuel Sanga, amekiri kumpokea mwanafunzi huyo jana saa kumi za jioni akiwa na majeraha mawili katika paja lake la kulia, akivuja damu nyingi na kumpatia matibabu ya dharura ili kuzuia damu zisiendelee kuvuja.

Chanzo: eatv.tv