Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi ahofiwa kufa kwa kuzama mtoni

Mwanafunzi ahofiwa kufa kwa kuzama mtoni

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Haruna Muya (14), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwaluguru  anadaiwa kufariki dunia baada ya kuzama katika mto Msangazi jana jioni Alhamisi Oktoba 31, 2019.

Juhudi za kumtafuta zinafanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi.

Diwani wa Kwaluguru,  Ramadhan Muya amesema mwanafunzi huyo ni mjukuu wake, kwamba alipotoka shule alikwenda kufanya  mazoezi  na baadaye kuanza kuogelea mtoni na wenzake.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni,  Godwin Gondwe amesema juhudi za kumtafuta mwanafunzi huyo zinaendelea, hadi leo saa 3 asubuhi alikuwa hajapatikana.

Amewataka viongozi na walimu kuwazuia watoto kuogelea katika maeneo yenye maji mengi.

“Msione hakuna mvua mkadhani hakuna maji mengi, mvua inaweza kunyesha maeneo mengine  na maji kujaa maeneo yetu. Kamati zote za maafa simamieni hili kuhakikisha watoto hawafiki katika maeneo hatarishi,” amesema Gondwe. Mpaka sasa  watu 16 wamefariki dunia wilayani Handeni baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Tanga na mikoa jirani.

Chanzo: mwananchi.co.tz