Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi afariki ndani ya bwawa, mwingine ajifyatulia risasi kidevuni

89833 Vifo+pic Mwanafunzi afariki ndani ya bwawa, mwingine ajifyatulia risasi kidevuni

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Watu wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania katika matukio mawili tofauti likiwamo la Epimark Ombela (61) kudaiwa kujipiga risasi.

Tukio la pili ni Peter Mushi (13) ambaye ni mwanafunzi na mkazi wa Shinga Wilaya ya Moshi kuteleza na kuangukia kwenye bwawa wakati anakata kuni pembezoni mwa bwawa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 24, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema tukio la mtu kujipiga risasi, lilitokea jana Jumatatu saa 12 asubuhi eneo la Kirua Vunjo Wilaya ya Moshi.

Kamanda huyo amesema mazingira ya tukio hilo kwamba marehemu alikutwa amejipiga risasi kwa kutumia bunduki aina ya Rifle yenye namba OC45451 ambapo aliiweka chini ya kidevu na kufyatua risasi iliyotokea kichwani utosini na kusababisha kifo chake.

"Chanzo cha kujiua kwa mtu huyo kinachunguzwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC," amesema Kamanda.

Kuhusu tukio la mwanafunzi, Hamduni amesema lilitokea jana Jumatatu saa 11:30 jioni, wakati mtoto huyo anakata kuni na kwamba mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya KCMC wakati uchunguzi zaidi ukifanyika.

Chanzo: mwananchi.co.tz