Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi afariki akiogelea

OGELEA.png Mwanafunzi afariki akiogelea

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: Mwananchi

Mwanafunzi wa chuo cha ufundi stadi Veta Kihonda Manispaa ya Morogoro, Martin Mushi mwenye umri wa miaka 21 amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea wenye bwawa lililopo jirani na chuo hicho.

Akizungumzia tukio hilo leo Oktoba12, Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro, Goodluck Zelote amesema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 10 saa moja jioni, ambapo mwanafunzi huyo alizama baada ya maji kumshinda nguvu.

Alisema kuwa kikosi cha waokoaji kilifika katika bwawa hilo akini ilishindikana kumuokoa mwanafunzi huyo kwa wakati kutokana na giza.

Hata hivyo, amesema waokoaji hao waliupata mwili wa marehemu asubuhi ya Oktoba 11 kuupeleka hospitali ya ajili ya uchunguzi wa kidaktari.

Kufuatia tukio hilo, Kamanda Zelote amewataka wanafunzi na wananchi wanaoishi jirani na bwawa hilo kuwa makini wanapochota maji, kuogelea au kufua katika anao hilo.

Chanzo: Mwananchi