Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi (14) ajinyonga kisa kulazimishwa kwenda kusoma kijiji kingine

NYONGA Mwanafunzi (14) ajinyonga kisa kulazimishwa kwenda kusoma kijiji kingine

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi Saada Ngedea(14) wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Shinamwenda Mkoani Geita amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba ya mti ambayo aliifunga kwenye mti.

RPC wa Geita Henry Mwaibambe amesema chanzo cha kifo ni kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa analazimishwa kutoka Kijijini wao na kwenda Kijiji cha Shinamwenda kusoma kwa kutembea kwa miguu baada ya baiskeli yake kuharibika ndipo alipokasirika na kwenda kujinyonga.

"Chanzo cha kifo ni kwamba Mwanafunzi huyu alikuwa analazimishwa kwenda Kijiji jirani kusoma kwa miguu baada ya baiskeli yake kuharibika ndipo alikasirika na kwenda kujinyonga"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live