Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MwanaApolo afariki dunia, wanne wajeruhiwa machimboni

50274 Pic+mirerani

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mererani. Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite maarufu mwanaApolo wa mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, amefariki dunia na wenzake wanne kujeruhiwa baada ya kudondokewa na viroba vya mchanga mgodini.

Kamanda wa polisi wa mkoani Manyara, Augostino Senga akizungumza mjini Babati jana Jumanne Aprili 2, 2019 amesema tukio hilo limetokea saa 4:00 usiku wa Machi 31, 2019 kwenye machimbo hayo.

Senga amemtaja aliyekufa kuwa ni Victor Lema (22) mkazi wa kijiji cha Mikungani kata ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Amesema mchimbaji huyo alikuwa anafanya kazi kwenye mgodi wenye PML namba 00003276 unaomilikiwa na Yuyuu Kasago mfanyabiashara wa Mererani.

Amesema majeruhi ni Baraka Japhet (24), Damian Martin (27), Shadrack Elitael (21) na Ernest Athanasio (20) ambao wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru).

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni viroba vya udongo uliokuwa unavutwa na mashine kudondoka wakati ukitolewa mgodini.

Hata hivyo, Senga amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hakuna mtu anayeshikiliwa kutokana na ajali hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz