Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu wa Madrasa atupwa jela miaka 30 kwa ulawiti

Pingu Law Mwalimu wa Madrasa atupwa jela miaka 30 kwa ulawiti

Sat, 16 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa mwalimu wa madrasa katika Msikiti wa Ushirika wilayani hapo, Abdalah Selemani (37), baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 12.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Nasra Mwashee ambaye alisema mahakama imeridhika bila kuacha shaka na ushahidi uliotolewa kuhusu kitendo hicho ambacho ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 154(1) (a) cha Kanuni za Adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwake na watu wengine wenye tabia ya kufanya vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto kwenye jamii na kuongeza kuwa ukatili kwa watoto hasa ubakaji na ulawiti, vimekuwa vikitokea mara kwa mara kwenye wilaya ya Nzega na adhabu hizo zitakuwa ni fundisho kwa wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live