Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu na mlinzi wa shule waliomjeruhi mwanafunzi kwa kipigo wakamatwa

Raulence Nicholous Mwanafunzi.jpeg Raulence Nicholous

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili akiwemo mwalimu wa Sekondari ya Loiler iliyopo mji mdogo mbalizi, Peter Emmanuel (29) na mlinzi wa shule hiyo Haruna Issa (30) kwa tuhuma za kumcharaza viboko mwanafunzi wa kidato cha IV sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwanafunzi huyo anaefahamika kwa jina la Raulence Nicholous (16 ) alituhumiwa kuiba maandazi matano katika duka la shule.

Mapema Februari 12, 2023 watumishi hao wawili wa shule hiyo walipobaini maandazi hayo matano yenye thamani ya Tsh 1500 yamepotea, ndipo walipotoa adhabu hiyo kali kwa mtoto huyo.

Waliohusika na tukio hilo baada ya kuona hali ya mwanafunzi huyo waliemcharaza fimbo si shwari walimkimbiza hospital ya Ifisi kwa ajili ya matibabu.

Pia, Kamanda wa Polisi amebainisha sababu ya mtoto huyo kuiba maandazi hayo kuwa ni njaa huku akilaani vikali adhabu iliyotolewa, na upelelezi wa shauri hili ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Baadhi ya wananchi Mkoa wa Mbeya wamelaani vikali kitendo cha walimu kuwapa adhabu nzito na za kupindukia wanafunzi mpaka kuwajeruhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live