Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu aomba msaada wa matibabu ya figo

59064 Figopic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Gharama kubwa ya matibabu ya figo na kukosekana kwa ndugu wa kumtolea figo kumemfanya, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kleruu mkoani Iringa,  Charles Kisese kuanza kuomba msaada ili anusuru uhai wake.

Mwalimu Kisese amesema kutokana na hali mbaya aliyonayo kwa sasa ameshauriwa kutumia dawa mpya ya kuzalisha seli ambayo inauzwa Sh1.45 milioni kwa dozi tatu.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Machi 22, 2019 mwalimu Kisese ambaye kwa sasa mwili wake umevimba amesema kwamba anahitaji msaada ili aweze kuanza matibabu ya dawa za kuzalishia seli.

“Mwili wangu unavimba kila kukicha na imebidi nihamie hapa Dar es Salaam ili nitibiwe, japo kila baada ya siku tatu nafanyiwa ‘dialyses’ nimeambiwa ninunue hizo dawa,” anasema.

Mwalimu Kisese amesema kutokana na gharama kubwa ya matibabu ya figo imekuwa vigumu kwake kumudu gharama hizo kwa sababu, bima imeshindwa kutosheleza.

“Atakayeguswa naomba anisaidie kupitia namba 0755811967  na ninaamini nikipona nitarudi kazini kuendelea kutekeleza majukumu yangu katika kuwafundisha wanafunzi,” anasema Mwalimu Kisese.

Pia Soma

Dalili na utambuzi wake.

Daktari kutoka Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila, Shindo Kilawa anasema dalili za magonjwa ya figo hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine.

Kilawa anasema kuongezeka kwa kisukari, shinikizo la damu, unene zaidi, uvutaji wa tumbaku na mafuta mengi mwilini ni kati ya sababu za kuongeka kwa ugonjwa wa figo ambao wataalamu wanasema bado sayansi ya matibabu haina tiba yake.

Anasema mara nyingi huwa inategemea eneo ugonjwa ulipo na mara nyingi dalili huwa za jumla na hazidhihiriki vyema.

Anataja dalili kuwa ni kuvimba uso, kichefuchefu, kukosa hamu ya chakula, kutapika, ukosefu wa damu, shinikizo la damu na mwili kuwa dhaifu.

“Japo mtu anaweza kuwa na dalili nilizotaja lakini haimaanishi kuwa kila dalili hizo ni ugonjwa wa figo kwa hiyo mtu akiona yupo kwenye hali hiyo anapaswa kupata matibabu,” anasema Dk Kilawa.

Chanzo: mwananchi.co.tz