Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu aliyesambaza picha wanafunzi wamekaa chini yamkuta

Madawarti D Mwalimu aliyesambaza picha wanafunzi wamekaa chini yamkuta

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa kazi na kuagizwa akamatwe na kwamba shule hiyo haina uhaba wa madawati.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live