Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Bariadi kimelaani tukio la Mwalimu wa shule ya msingi Nyamagana Lucia Shirima kuvamiwa na kukatwa vidole viwili ambapo kati ya vidole hivyo kidole kidogo cha mkono wa kulia kilidondoka kwenye uvungu wa kitanda huku kidole gumba cha mkono wa kushoto kikiwa kimening'inia.
Viongozi wa CWT wakiwa nyumbani kwa Mwalimu huyo wamesema baadhi ya wanajamii hawaoni umuhimu wa walimu kuwa kwenye maeneo yao hivyo ni vema wakaelimishwa kuachana na vitendo vya kikatili dhidi ya walimu.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Agosti 24, 2023, ambapo Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu limethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio hilo na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.