Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu adaiwa kujiua kwa sumu

71971 Pic+mwalimu

Mon, 19 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Sekondari ya Mbalamaziwa, Roida Mbalwa amefariki dunia kwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa mkutano na kiongozi mmoja kutumia fedha vibaya za ujenzi.

Mume wake, Sharif Utenga alisema kiongozi huyo alifanya mkutano wa hadhara kata ya Mbalamaziwa na wananchi walieleza kuchangishwa michango mingi.

“Ninachokifahamu alikuja (anamtaja) alizungumza na wananchi walidai michango imekuwa mingi kitu ambacho kiliamsha kwenda kumkagua mwalimu baada ya ukaguzi waligundua kuna hasara takriban Sh200 milioni,” alisema Utenga.

Alisema mara kwa mara wakaguzi wa halmashauri ya Mufindi walikuwa wakifika shuleni na kukagua ujenzi kwa sababu majengo hayo yanatarajia kuzinduliwa na Mwenge.

“Mke wangu alikuwa akipata presha ya kazi kutoka kwa viongozi waliofika kuwa wakali na kumtuhumu kutumia fedha vibaya, alikuwa akiwaambia walimu wenzake kuwa ipo siku nitakuja kujiua,” alisema Utenga.

Hata hivyo, diwani wa Mbalamaziwa Zubeir Nyamolelo alisema mwalimu huyo hajawahi kutuhumiwa kwa lolote.

Pia Soma

“Mikutano yote nilikuwa na (kiongozi huyo) hakuwahi kumtuhumu kwa ubadhilifu na hakuna mkaguzi yeyote aliyewahi kuja,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema mwalimu huyo waliyemzika jana walikuwa wanamtegemea na amefanya kazi vizuri kwa miaka 12.

“Sina taarifa yoyote ya matumizi mabaya ya fedha ambayo inaweza kusababisha anywe sumu, hapana kabisa!” alisema William.

Mmoja wa walimu wa shule hiyo, Philipo Mkandawile alisema kifo hicho kilitokea Jumatano iliyopita.

Chanzo: mwananchi.co.tz