Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu adai kulazimishwa na Mwalimu mkuu kuishi darasani

Darasa ?fit=700%2C400&ssl=1 Mwalimu adai kulazimishwa na Mwalimu mkuu kuishi darasani

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa shule ya msingi Lemosho Kata ya Endument mkoani Kilimanjaro, Stephano Nyambuyu analazimika kuishi kwenye chumba cha darasa la shule hiyo, akidai kuzuiwa kuishi kwenye nyumba ya shule na Mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Asantaeli Sandewa akijibu malalamiko hayo, amesema nyumba inayodaiwa kuwa wazi ina mwalimu na ambaye ni mke wa mtu.

Malalamiko hayo yametolewa leo Desemba 16 na mwalimu huyo shuleni hapo baada ya kamati ya utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kufika shuleni hapo wakifanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo Stephano alisema amekaa akiishi hapo darasani kwa miezi miwili pia akiwa anapikia nje hali ambayo mvua ilinyesha amekuwa akishindwa kupika na kushinda na njaa. "Nimehamia kutoka Wila ya Ngara mkoani Kagera kuja Wilaya ya Siha ambapo nimebadilishana kituo cha kazi na mwalimu mwingine, hivyo nimekuja katika shule hii ninaishi darasani. “Huu ni mwezi wa pili na kuna nyumba haina mtu, lakini kila nikimweleza mwalimu mkuu anipe nyumba hiyo iliyofungwa amekuwa hanielewi. Anasema hiyo nyumba hutakiwi kuingia endelea kijibana kukaa hapo darasani,” amesema.

Ameongeza kuwa, ameshindwa kubisha na mkuu wake wa kazi licha ya adha anayopata. “Wanafunzi wamekuwa wakichungulia sehemu ninayoishi darasani. Nimekuwa nikifedheheka sana,” alisema mwalimu huyo. Mwenyekiti wa Shule hiyo, Shabani Hasani alikiri kufahamu uwepo wa mwalimu huyo kukaa darasani huku, anasema hii sio sahihi mwalimu kuishi darasani tutafanya utaratibu wa kuhakikisha mwalimu anapewa nyumba,

Akijibu malalamiko hayo, Mwalimu Mkuu Sendewa amesema mwalimu huyo ametoa taarifa za uongo, kwani nyumba anayoisema ina mwalimu ambaye ni mke wa mtu na yupo likizo. “Sasa hatuwezi kuweka mke wa mtu na mume wa mtu kwenye nyumba mmoja, hivyo tunafanya utaratibu,” alisema Sendewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live