MWENYEKITI wa Bodi ya Dawasa, Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange amesema , wataendelea kutekeleza miradi mkubwa na midogo kwa wakati ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa asilimia 100 kabla ya mwaka 2025.
Huku akishangiliwa, Jenerali Mwamnyange amesema “nawapenda sana wafanyakazi wa Dawasa. Naipenda Dawasa kutoka moyoni. Tangu nilipoteuliwa kuwa mwenyekiti nimeshuhudia uzalendo, ujasiri, ushirikiano kwa kweli ninyi ni bora.”
Jenerali huyo mstaafu amesema “ningeweza au natamani Dawasa lingekuwa na jina la pili vilevile kwamba Dawasa liitwe jina la pili Jeshi la Huduma ya Maji kwa Wananchi ya Dar es Salaam na Pwani.”
“Wananidhamu sana na CEO (Luhemeja) ningetamani awe na jina la pili, Mkuu wa Jeshi la Huduma ya Maji.
Akitoa maelezo ya upatikanaji wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema, kwa sasa upatikanaji wa maji kwa maeneo wanayoyahudumia ni asilimia 92 “na malengo yetu ifikapo Juni 2023 tuwe tumefikia maeneo yote kwa asilimia 100.”
Amesema, kwa sehemu kubwa, wanatumia fedha za ndani kugharamia miradi mbalimbali mikubwa na midogo lengo ni kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati ili kufikia malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).