Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvutano wa utendaji mamlaka za Serikali washtua wajumbe wa bodi ya barabara

Mvutano wa utendaji mamlaka za Serikali washtua wajumbe wa bodi ya barabara

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Songwe, wamezinyooshea kidole Wakala wa Barabara mijini na vijijini (Tarura), Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) na Uwasa kutokana na kushindwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za mitaa kwa madai kuwa zinawajibika Wizarani.

Hilo limesemwa leo Alhamisi Februari 13, 2020 na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mercia Swela katika kikao kazi cha baraza hilo. Swela amesema wakala hizo ambazo awali zilikuwa chini ya halmashauri, baadaye ziligeuzwa na kuwa wakala zinazojitegemea, hivi sasa zimejitenga na hazitoi ushirikiano kwa halmashauri wala mamlaka nyingine za serikali, hali inayofanya madiwani washindwe kujua mpango kazi wao, kwa madai zinaripoti moja kwa moja wizarani.

Makamu Mwenyekiti huyo amesema kutokana na hali inasababisha madiwani kushindwa kujua utekelezaji wa miradi inayoendelea na hata bajeti zao hazijulikani na hawahudhurii hata vikao vya madiwani.

Mbunge wa Tunduma, Frenk Mwakajoka amesema wakala hizo zinakwepa majukumu yake kwa kujitenga na halmashauri, kitendo ambacho kinawanyima fursa madiwani kusimamia miradi iliyopo katika maeneo yao.

“Tarura watambue kwamba halmashauri zimekuwa zikitenga fedha kwa ajili ya barabara, fedha hizo hazitumiki kulingana na uhusiano mbaya uliopo,” amesema Mwakajoka.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila amesema kuziondoa wakala hizi toka serikali za mitaa haimanishi kuondoa uhusiano.

Pia Soma

Advertisement
Alisema miongozo inaagiza taasisi yoyote ya serikali iliyopo wilayani, inapaswa kuwajibika kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali.

“Someni vizuri standing older na yeyote ambaye ataendelea kukaidi hili, hatua za kawaida za kinidhamu zitachukuliwa,” amesema Kafulila.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz