Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvumbuzi wa Tanzanite kuzikwa Jumamosi

39426 Mzee+pic Mvumbuzi wa Tanzanite kuzikwa Jumamosi

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma unatarajia kusafirishwa kesho Ijumaa Februari mosi 2019 kwenda Kijiji cha Makanya, wilayani Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 31, 2019 binti wa marehemu, Asha Ngoma amesema kwa sasa msiba upo Mbezi Maramba mawili jijini Dar es Salaam na mwili umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mzee Ngoma alifariki dunia jana Jumatano kwenye MNH alikokuwa akipatiwa matibabu.

“Tunatarajia kuzika siku ya Jumamosi huko Makanya,  Kilimanjaro, tutasafiri kesho. Ratiba inaonyesha taratibu zote za kuutayarisha mwili kwa ajili ya safari zitafanyika msikiti wa Maamur Upanga,” amesema Asha na kuongeza:

“Hatujajua kama tutakuwa na utaratibu wa kuaga, kama tutapata mahali kwa ajili ya shughuli hiyo tutatoa taarifa.”

Mzee Ngoma alikabidhiwa Sh100 milioni na Rais John Magufuli Aprili mwaka jana kwa ajili gharama za matibabu yake na matumizi mengine.

“Zile Sh100 milioni alishakabidhiwa mwezi uleule wa nne, kilichobaki ni cheti na mazungumzo kama ambavyo Rais alisema akatibiwe kwanza kisha atamkabidhi cheti na watazungumza,” amesema Asha.

 

 

 

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz