Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua zasitisha usafiri wa mwendokasi kupitia Jangwani

56037 Jangwani

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mvua zinazoendelea kunyesha zimesitisha huduma za usafiri katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) kwa mabasi yake yanayopitia daraja la Jangwani.

Kwa wanaotumia mwendokasi kupitia Morocco usafiri uko kama kawaida hivyo kwa wale tu wanaopitia Jangwani ndiyo watashindwa kwa kuwa daraja la Jangwani lililopo barabara ya Morogoro limefungwa kutokana na kufurika maji.

Mkurugeni Mtendaji wa Udart, John Nguya amesema kuwa kutokana na daraja hilo kujaa wale abiria wote wanaoenda Posta, Kivukoni na Kariakoo inabidi washukie Magomeni na kutafuta jinsi ya kufika maeneo hayo.

Amesema kuwa walifanya utaratibu wa dharura ili wanaoenda Kivukoni wafikishwe Morocco halafu Sumatra waandae mabasi ya kufikisha maeneo hayo lakini bado maji ni mengi.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Redio Clouds Fm, Bonge daraja hilo limefurika maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa.

Akizungumza leo Mei Jumaane 07, 2019, Bonge amesema kuwa, kutokana na daraja hilo kujaa maji watumiaji wa barabara hiyo wanaweza kutumia barabara mbadala ili kuendelea na shughuli zao.

Mvua zimeendelea kunyesha jijini hapa zilianza Mei 04, 2019 na zinaendelea hadi leo.



Chanzo: mwananchi.co.tz