Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua zakata mawasiliano barabara ya Morogoro

Mvua Barabaraaa (600 X 346) Mvua zakata mawasiliano barabara ya Morogoro

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro zimeharibu na kukata mawasiliano ya barabara inayoingia Chuo Kkuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Solomoni Mahlangu na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo wamesema hii si mara ya kwanza kwa mawasiliano ya barabara hiyo kukatika, na hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa maji yanayotoka mto Ngerengere.

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Morogoro unaendelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live