Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yazua jambo Serengeti, yaezua paa shule ya msingi Singisi

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Wanafunzi 284 wa Shule ya Msingi Singisi Wilaya ya Serengeti hawana mahala pa kusomea baada ya mvua iliyoambata na upepo mkali kuezua paa la madarasa matatu na ofisi ya walimu.

Tukio hilo limetokea juzi Alhamisi Agosti 29, 2019.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo,  Vicent Okwaro amesema madarasa hayo kukosa paa kumeathiri wanafunzi wa darasa la kwanza, nne, tano na walimu wanane ambao kwa sasa wanalazimika kutumia ofisi moja ya mwalimu mkuu.

"Tumefunga shule kwa wiki moja, wanafunzi wa darasa la saba na la tano ndio wamebaki, wengine wakifungua shule kama kutakuwa hakujafanyika ukarabati sijui itakuwaje," amesema.

Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho,  Magatini Mambolele amesema wamelazimika kuitisha mkutano kuweka mkakati wa kuanza ukarabati na kuomba wadau mbalimbali kuwasaidia.

Chanzo: mwananchi.co.tz