Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaua watu 11 Tanga

81823 Mvua+pic

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Watu 10 wamefariki dunia wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika shimo baada ya barabara ya Handeni-Korogwe eneo la Kindeni kusombwa na maji.

Wakati gari hilo likisombwa na maji, mwingine amefariki dunia katika eneo hilo akiwa katika jitihada za kuvuka eneo lililojaa maji.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26, 2019 mkuu wa Wilaya ya Handeni

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema watu 10 wamefariki baada ya gari kutumbikia katika shimo lililotokana na barabara kusombwa na maji, mwingine kusombwa na maji.

Tangu jana Ijumaa Oktoba 25, 2019 mamia ya abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani kuelekea Dar es Salaam na waliotoka Dar es salaam kuelekea mikoa mbalimbali walikwama katika eneo hilo.

Mbali na watu hao kufariki dunia  baadhi ya kaya zililazimika kuhama makazi yao kwa muda katika Wilaya ya  Korogwe kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Nyumba hizo zilianza kujaa maji baada ya mto Pangani kufurika na maji kuanza kuelekea katika makazi ya watu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz