Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaua watoto wawili Same

Mvua Pc Data Mvua yaua watoto wawili Same

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia alfajiri ya leo Desemba 11, baada ya nyumba yao waliokuwa wamelala kuangukiwa na kifusi cha udongo kufuatia mvua kubwa kunyesha katika Kijiji Cha Mhero Kata ya Chome wilayani Same.

Katika tukio hilo watu wengine watatu wamejeruhiwa ikiwa  watoto wawili wa familia hiyo pamoja na mama ya mzazi.

Akizungumzia tukio hilo diwani wa Kata hiyo ya Chome Herieli Bonifasi Makange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema usiku wa kuamkia leo mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo na kuharibu mali za wananchi.

"Tumepatwa na maafa makubwa ndani ya Kata hii mashamba yenye mimea mbalimbali yamezolewa barabara zimefungwa wananchi wamekwama kusafiri leo,” alisema"

Akizungumzia matukio hayo mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo ya Same, Yusto Mapende amesema mvua hizo zimeleta athari mbalimbali ndani ya wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa barabara  kuu ya Dar-Arusha ambayo ilifungwa na maji katika eneo la Makanya.

Mapande amesema sambamba na barabara hiyo pia barabara zingine ndani ya wilaya hiyo zimefungwa na vifusi na daraja la Saseni huko katika Kata za Bwambo na Kirangare kukatika.

Advertisement Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limethibitisha kutokea kwa maafa hayo na litatoa taarifa kamili kupitia kwa kamanda wa polisi mkoani hapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live