Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaua watatu Iringa

Mvua yaua watatu Iringa

Tue, 28 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Watu watatu wamekufa huku kaya 62 zikikosa makazi kutokana na mafuriko yaliyokikumba kijiji cha Tungamalenga na Idodi wilayani Iringa Mkoa wa Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 27, 2020 mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wamekufa watu watatu, wakiwemo watoto wawili.

Amesema watoto hao nyumba wanayoishi ilizingirwa na maji, wakati wakitoka nje mama yao alishika mti na hakusombwa na maji.

“Watoto hawakushika mti wakasombwa na maji, mwili wa mtoto mmoja na mtu mwingine tumeipata, wamezikwa ila tunaendelea kutafuta mwili wa mtoto mwingine,” amesema Kasesela.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema eneo la Pawaga nyumba takribani 41 zimebomoka na nyingine za tarafa ya Idodi zimeathiriwa na mvua kwa kiasi kikubwa.

“Niwashukuru wenyeviti wa vijiji hivyo kwa kuwaunganisha wananchi waliokumbwa na mafuriko na kuwaweka katika nyumba ambazo hazijazingirwa na maji,” amesema Kasesela, akibainisha kuwa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa Ruaha kupitia Msembe Tungamalenga haipitiki.

Pia Soma

Advertisement
Amewataka wananchi wa vijiji vya Pawaga na Idodi kuhama katika maeneo yenye mkondo wa maji.

“Gereza la Pawaga limezingirwa na maji, tunaangalia hali ya leo na kesho kama maji yatazidi tutawahamisha wafungwa kuwaleta gereza la mjini,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz