Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaua mmoja Musoma

Mvua yaua mmoja Musoma

Sun, 1 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Mvua inayoendelea kunyesha manispaa ya Musoma kuanzia leo asubuhi Jumamosi Novemba 30, 2019 imesababisha kifo cha mtu mmoja na mwingine kujeruhiwa.

Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk Vicent Naano amesema aliyefariki hajafahamika lakini alikuwa mkazi wa mtaa wa Mshikamano manispaa ya Musoma.

Amesema amefariki dunia baada ya kusombwa na maji.

Amesema mvua hiyo imeharibu mali mbalimbali za wananchi, " majeruhi amekimbizwa katika hospitali ya Mkoa kwa matibabu."

Amesema tathmini ya athariĀ  ya mvua hiyo inayonyesha zaidi wilayani Butiama imeanza, akisisitiza kuwa taarifa kamili itatolewa kesho.

Chanzo: mwananchi.co.tz