Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yasomba barabara Shinyanga

88132 Pic+mvua Mvua yasomba barabara Shinyanga

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga.  Mvua iliyoanza kunyesha jana Jumanne Desemba 10, 2018 mkoani Shinyanga imesababisha wakazi wa kata ya Mwakitolyo kuvushwa kwa mtumbwi kutoka upande mmoja kwenda mwingine baada ya barabara kusombwa na maji.

Wakazi wa kata hiyo walilazimika kulipa Sh2000 ili kupanda mtumbwi huo huku waliokosa kiasi hicho cha fedha wakibaki kuwa watazamaji.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 11, 2019 mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amefika eneo hilo na kushuhudia adha wanayoipata wananchi.

Aliwataka kuwa watulivu wakati taratibu nyingine zikiendelea kufanywa na kuwatahadhalisha wenye mitumbwi kutobeba watu wengi.

"Hali si nzuri barabara imekatika hakuna mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda mwingine, wananchi kama unavyoona wanabebwa kwa mitumbwi ila nimewapa tahadhari wasiweke tamaa mbele wabebe watu wachache,” amesema mkuu huyo wa Wilaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz