Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yasababisha hasara ya Sh8 milioni mkoani Mbeya

78823 Pic+vifo

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mvua iliyonyesha jana Jumapili Oktoba 6, 2019 na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo mjini Mbeya imesababisha hasara ya Sh8.8 milioni baada ya kusombwa kwa mabomba katika chanzo cha maji kata ya Ivumwe.

Hasara hiyo iliyopata Mamlaka ya Maji safi na Usafi Wa Mazingira Mkoa Wa Mbeya (UWSA) imesababisha asilimia 30 ya wakazi wa mji wa Mbeya kukosa huduma ya maji safi na salama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo,  Ndele Mengo amelieleza Mwananchi leo Jumatatu Oktoba  7, 2019  kuwa chanzo hicho cha maji kilikuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita 10 milioni kwa siku na kusambaza kwa asilimia 30 kwa wateja wa Mbeya na Mamlaka ya Mji mdogo Wa Mbalizi wilaya ya Mbeya.

"Tumepata janga kubwa  kwani chanzo hicho ni miongoni mwa vyanzo tegemezi lakini kama mamlaka kwa sasa tuko katika maeneo yaliyoathirika katika kufanya matengenezo ili kurejesha huduma hiyo kwa wananchi ambayo kwa sasa imesitishwa kwa muda na kwamba bomba lililopasuka lina ukubwa wa nchi 19,” amesema.

Ofisa mahusiano wa mamlaka hiyo,  Neema Stanton amewaonya wananchi kutokimbilia maeneo yenye mafuriko pindi yanapojitokeza kwa lengo la kunusuru Usalama  Wa maisha yao.

Amesema kumekuwepo na kasumba ya wananchi kukimbilia maeneo ambayo wanasikia kuna changamoto hususan mafuriko na moto bila kujali kuna uwezekano wa  kupata madhara ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai .

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz