Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaleta maafa Dodoma, mtu mmoja afariki

Mvua Makarani Mvua yaleta maafa Dodoma, mtu mmoja afariki

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua kubwa iliyonyesha jana jioni mkoani hapa imeleta maafa na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mifugo katika Mtaa wa Mchemwa.

Akizungumza leo Desemba 21, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makutupora, Hamisi Jigwa amethibitisho kifo cha moto Sarah Meso (4) aliyekutwa na mauti baada ya kuangukiwa na paa la nyumba waliyokuwa wanaishi huku mtoto mwingine akijeruhiwa.

"Ni kweli tukio hilo lipo katika Kata yangu Makutupora katika Mtaa wa Azimio huku Mchemwa, taarifa za uharibifu zaidi mtazipata kwa mamlaka bado nazikusanya,” amesema.

Jigwa amesema kwenye tukio kuna vifo vya mifugo ambayo hadi asubuhi mifugo iliyokufa ni mbuzi 15 na ng'ombe watatu.

Zingine ni idadi ya nyumba ambazo hazi sasa haijajukikana kwani serikali ya Mtaa na Kata wanaendelea kukusanya taarifa zake.

Aksa Lubeleje amesema mifugo mingi imekufa kwani mvua ilinyesha majira ya jioni wakati mifugo ikiwa machungani ambako mara nyingi huwa inaongozwa na vijana lakini jana hiyo haikurudishwa kutoka porini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live