Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakwamisha wanafunzi kuhudhuria masomo Mtwara

C09182ab7b1f373ce20b3114da1da53b Mvua yakwamisha wanafunzi kuhudhuria masomo Mtwara

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADHI ya wanafunzi Mkoani Mtwara wameshindwa kwenda shule kutokana na mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha huku baadhi ya wananchi wakilazimika kuhama makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji.

Mkuu wa Mkoa Gelasius Byakanwa amesem hayo leo wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama wa wananchi na makazi yao kufutatia mvuo kubwa ambayo ilianza kunyesha nyuzi usiku.

Amewata wananchi ambao makazi yao yapo katika maeneo ya hatari na yenye matatizo ya mafuriko kuhama na kwenda katika sehemu zilizotengwa kwa ajili ya usalama wao.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba mvua zinaendelea kunyesha na wito wangu kwa wananchi ni kuendelea kuchukua tahadhali na tunawamasisha kutoka kwenye maeneo tuliyoyatenga kwa ajili ya usalama wao,” amesema.

Amesema kutoka na hali hiyo ambayo pia imepelekea baadhi ya wananchi kuhama makazi yao, imesababisha baadhi ya watoto kushindwa kwenda shule huku akiahidi kuhakikisha wanafunzi wote wanaenda shule baada ya hali ya hewa kutengemaa.

Kwa hatua nyingine, Byakanwa amesema mvua ambayo imenyesha jana imeonyesha kwamba kuna tatizo la kiutalaam katika kujenga barabara ambapo hawazingatii ‘photography’ huku akiwata TARURA na Tanroads kujichunguza na utaalam wao katika kuhakikisha ujenzi bora wa barabara kuzuia mafuriko.

RC huyo amesema barabara nyingi mkoani hapa zimefungwa hazipitiki kutokana na maji kutwama.

“TARURA wanao ‘assignment’ barabara nyingi zimefungwa hazipitiki, kuna tatizo la kiutalaam--kun uhitaji wa kujichunguza na utaalam wa design za barabara zetu,” amesema.

Katika hatua nyingine Byakanwa ametoa pole kwa wakazi ambao wameathirika na mvua hizo na kwa familia ambayo ilipoteza kijana wao “Bodaboda” ambaye alikuwa akakatisha katika maji ambayo yalijaa barabarani.

Amesema uongozi wa mkoa unaendelea kuthibiti hali kwa kutoa tahadhali kwa wananchi ambao wako kwenye maeneo ya hatari na matatizo makubwa ya mafuriko.

Ametaja baadhi ya sehemu ambazo zimeathirika na mvua kuwa ni Naliendele, Ligula, Kiangu, Matopeni, Likole, Chipuputa na Maramba Wilani Mtwara.

Chanzo: habarileo.co.tz