Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakata mawasiliano ya Serengeti- Bunda Tanzania

90082 Mvua+pic Mvua yakata mawasiliano ya Serengeti- Bunda Tanzania

Sat, 28 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mvua inayoendele kunyesha Mkaa wa Mara nchini Tanzania, leo Alhamisi Desemba 26,2019 imesababisha kusobwa na maji daraja la Issenye linalounganisha Wilaya za Serengeti na Bunda mkoani humo. Hali hiyo imesababisha adha kwa watumiaji wa barabara hiyo kutokana na kutokuwapo kwa uwezokano wa kupita kwa mtu au chombo chochote cha usafiri kwa zaidi ya saa 4. Mbunge wa Serengeti (CCM), Marwa Ryoba akiwa eneo la tukio ameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia suala hilo kwa jicho la kipekee ili kuwawezesha wananchi na watalii kwenda na kurudi maeneo yao. "Serikali inatakiwa kuharakisha ujenzi wa barabara ya lami makutano ya Natta Mugumu ili kuondokana na matatizo kama hayo," amesema Ryiba "Serengeti ni wilaya yenye kivutio kikubwa cha Hifadhi yenye umaarufu mkubwa, mazingira kama haya yanaathiri utalii, daraja la Fort Ikoma limekatika,hapa ambapo ni kiungo cha wilaya mbili pia limekatika tunakuwa kisiwani,naomba walitizame kwa uzito," amesema Dreva wa basi la Imarejesho,Elisaidi Ayo amesema ubovu wa miundombinu unawaathiri kiuchumi pia unachangia magari kuharibika huku akiomba Serikali ya Tanzania kuitazama wilaya ya Serengeti kwa jicho la kipekee. Sospeter Nyigoti mmoja wa abiria waliokuwa wanakwenda Bunda amesema kwa hali ilivyo sasa hana uhakika wa kwenda na kurudi na gharama za kuzunguka Tarime ni kubwa. Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) mkoa wa Mara Reginald Massawe amesema kutokana na wingi wa mvua kazi za kutengeneza barabara zimesimama lakini wanahangaika kurekebisha madaraja ambayo hayapitiki ili kuwawezesha abiria kupita. Hadi saa 1 usiku magari yalikuwa hayajaanza kupita eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz