Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakata mawasiliano ya Bunda- Serengeti Tanzania

90199 MVUAPIC Mvua yakata mawasiliano ya Bunda- Serengeti Tanzania

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Abiria wa  kutoka Serengeti kwenda Bunda mkoani Mara nchini Tanzania na wakuingia wilayani humo wamekwama Issenye kufuatia maji ya mvua kusomba kifusi na mawe yaliyokuwa yamewekwa kwa muda kwenye daraja na kusababisha magari kushindwa kupita.

 

Hali hiyo imejitokeza leo Jumamosi Desemba 28, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya abiria kukwama hapo baada ya maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuharibu sehemu ya daraja.

Wataalam wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) walilazimika kufanya marekebisho ya muda na kuwezesha magari kuvuka.

 

Mmoja wa abiria kutoka Bunda jina limehifadhiwa ameliambia Mwananchi kwa simu kuwa kutokana na hali ilivyo hawawezi kupita mpaka maji yapungue ili waone wapi pameharibika.

"Inabidi waweke udhibiti mkali maana nimeshuhudia akina mama wawili wanapita kwa miguu wameshikana na mmoja ana mtoto ni hatari sana, maana haijulikani kama daraja lipo kwa kuwa maji mengi yanapita huu ya daraja," amesema.

 

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema madaraja mengi yana matatizo yanahitaji kutengenezwa vizuri baada ya mvua, kwa sasa  kazi inayofanyika ni marekebisho ya dharura.

"Hapo Issenye ni juzi tu watu wamekwama baada ya maji kupungua wakaweka mawe na kifusi magari yakapita, leo tena imejitokeza nasisitiza hasa madereva kuchukua tahadhari katika kipindi hiki," amesema.

Amesema daraja la Fort Ikoma limerekebishwa na magari yanapita ,"lile la Robana lilikuwa limeishakatika nusu nilikuwa huko na watu wa Tanroad wamejaza mawe na kudhibiti hali kwa sasa hatujui baadae maana mvua zinaendelea kunyesha."

Christian Nanak mkazi wa Issenye amesema miundombinu hadi vijijini imeharibika sana na wana wasiwasi kama mvua zinaendelea kunyesha mpaka kipindi cha kufungua shule baadhi ya watoto hawatahudhuria kutokana na mito mikubwa ambayo imeanza kuibuka maeneo mbalimbali .

"Wilaya hii kila mwaka wakati wa mvua tunapata matatizo kama haya, sijui kwa nini tumesahaulika namna hii licha ya fursa kubwa  za utalii zilizopo," amesema.

Desemba 25, 2019 mvua kubwa zilizonyesha  wilayani hapo zilisababisha vifo vya watu watatu, kujeruhi mmoja na madaraja kukatika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano ya Mugumu Fortikoma na Robanda.

Watoto wawili walikufa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba baada ya maji kujaa ndani katika kijiji cha Issenye na mmoja kujeruhiwa, huku mwendesha pikipiki mmoja akisombwa na maji baada ya kulazimisha kupita ndani ya maji yaliyokuwa yanapita juu ya daraja na wawili kunusurika wakati wakitoka kusherehekea sikukuu ya Krismasi Natta.

Chanzo: mwananchi.co.tz