Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakata mawasiliano Sengerema- Buchosa

Buchosa Mawasiliano (600 X 311) Mvua yakata mawasiliano Sengerema- Buchosa

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua iliyonyesha kwa saa nane wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza usiku wa kuamikia leo Jumatatu Novemba 27, 2023 imekatisha mawasiliano ya barabara ya Sengerema-Buchosa kwenye Kijiji cha Luchili wilayani humo.

Hali hiyo imesabisha abiria kukwama kwa saa tano huku wengine wakivushwa kwakutumia mitumbwi.

Baadhi ya wananchi wanaoitumia barabara hiyo wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kuwaondolea adha wanayoipata kutokana na mvua zinavyoendelea kunyesha.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga alipotafutwa kuzungumuzia suala hilo amesema anaelekea eneo la tukio kujionea hali halisi ya kukatika Kwa barabara hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live