Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yakata mawasiliano Mugumu –Musoma, abiria wakwama

86302 Mvuapic Mvua yakata mawasiliano Mugumu –Musoma, abiria wakwama

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Serengeti Mkoa wa Mara zimekata mawasiliano ya usafiri kati ya Mugumu na Musoma kutokana na maji kufunika barabara eneo la Kenyana.

Maji yalianza kujaa saa 2 asubuhi leo Alhamisi Novemba 28, 2019 na kusababisha magari kushindwa kupita.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu na katibu tawala, Cosmas Qamara ni miongoni mwa walioshindwa kupita eneo hilo wakati wakiwahi kikao cha mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima. Wamekaa eneo hilo zaidi ya saa moja huku maji yakizidi kuongezeka.

"Tumelazimika kurudi na kuzunguka njia nyingine ili tuwahi kikao, naomba wananchi wasifanye mzaha kuvuka na wale walioko kwenye mabonde wachukue tahadhari," amesema Babu.

Chanzo: mwananchi.co.tz