Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaharibu makazi ya familia 15

79213 Pic+mvua

Wed, 9 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Nyumba za familia zaidi ya 15 katika kijiji cha Kikungwi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja zimeharibiwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali.

Mvua hiyo pia imezoa mazao mbalimbali na kuharibu miundombinu ya barabara na umeme.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 9, 2019 mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amesema baada ya kutokea athari hiyo, wamewatembelea wananchi kuwapa pole.

Amewataka kuwa na subira na kwamba Serikali imeshatuma timu ya kufanya tathmini kuhusu maafa yaliyotokea na itatoa majibu ya nini kifanyike.

Amesema wananchi ambao hawana mahala pa kuishi, watapewa maeneo ya muda pamoja na chakula.

Mkuu wa Wilaya ya kati Unguja, Hamida Khamis Mussa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari kwa kutokaa chini ya miti katika kipindi hiki cha mvua na upepo mkali.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz