Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaharibu madaraja Kilosa

Madaraja Kilosa Mvua.png Mvua yaharibu madaraja Kilosa

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawasiliano ya barabara ya Dumila Kilosa Mjini yamekatika baada ya daraja la muda la Ilonga Msalabani na Mazinyungu kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima ametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mafuriko hayo na kuanzia TANROADS kurejesha mawasiliano ya barabara zilizofungiwa kwa haraka ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea.

Kufuatia mvua hizo madaraja manne yameharibikiwa na yamefungwa kutumika ikiwemo Daraja la Mto Mazinyungu, Mkondoa, Ilonga na Uhindini.

Kwa upande wake Menejea TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Lazack Kyamba amesema tayari wameshafanya tathmini ya athari iliyopo na watarajesha mawasiliano ya barabara ya Dumila -Kilosa pamoja na Mikumi -Kilosa ndani ya siku mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live