Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua ya upepo yaezua mapaa Misungwi

10097 PAA+PIC TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi. Mvua ya upepo iliyonyesha jana Ijumaa Agosti 3, 2018  katika kijiji cha Iteja Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imeezua paa za nyumba kadhaa ikiwemo vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Aimee Milembe iliyopo kijijni hapo.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 4, 2018 mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama waliotembelea kijiji hicho kukagua madhala ya mvua, mkuu wa shule hiyo, Florencia Ndubashe amesema vyumba vinne vya madarasa, ofisi ya walimu pamoja na vyumba viwili vya maabara vimeezuliwa paa.

"Hii ni mara ya pili miundombinu ya majengo katika shule yetu inaathiriwa na mvua ya upepo. Mwaka 2013 mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliezua paa ya vyumba viwili vya madarasa," amesema mwalimu Ndubashe.

Katibu tawala wa Wilaya ya Misungwi,  Marco Peter aliyeongozana na wajumbe wa kamati hiyo amesema taarifa kamili kuhusu madhala ya mvua zitatolewa baadaye na Mkuu wa wilaya hiyo, Juma Sweda baada ya kupokea taarifa itakayokusanywa na kamati.

Chanzo: mwananchi.co.tz