Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua ya mawe yamkwamisha Majaliwa kushuka kwenye gari

42426 Pic+mvua Mvua ya mawe yamkwamisha Majaliwa kushuka kwenye gari

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibondo. Mvua ya barafu imemzuia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushuka kwenye gari kuendelea na ratiba yake kukagua kituo cha afya na kuhutubia mkutano wa hadhara katika kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma.

Tukio hilo limetokea katika kambi ya wakimbizi Nduta, wilayani Kibondo majira ya saa 6:30 mchana leo Jumatatu Februari 18, 2019 ikiwa ni siku yake ya tatu katika ziara hiyo mkoani hapa.

Watu wote katika msafara akiwepo Waziri Mkuu wamelazimika kubaki kwenye magari ili mvua ipungue na ndipo waendelee na ratiba.



Chanzo: mwananchi.co.tz