Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua ya dakika 10 yaacha hasara ya mamilioni Mwanza

61041 MVUA+PIC

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mvua kubwa iliyoambatana na upepo , imeharibu bidhaa za Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake (TWCC), waliokuwa kwenye maonyesho ya bidhaa zao katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 02, 2019 katibu wa chemba hiyo,  Mary Mayala amesema mvua hiyo iliyodumu kwa dakika takribani 10 tu, imewasababishia hasara ya mamilioni (Bila kutaja kiasi halisi) wakati wakiendelea na shughuli zao za kijasiriamali.

"Tathimini inaendelea kufanyika, lakini ukweli ni kwamba tumepata hasara , maana karibia kila mtu hapa alikuwa na bidhaa tofauti, mfano wale wauza vinywaji kama 'wine’ (Mvinyo) chupa zimepasuka lakini pia vyombo vimesombwa na vingine kupasuka,” amesema Mayala.

Chanzo: mwananchi.co.tz