Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua kubwa kunyesha mikoa 18 Tanzania

97849 Mvua+pic Mvua kubwa kunyesha mikoa 18 Tanzania

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo katika mikoa 18 nchini humo kuanzia leo Jumanne Machi 3, 2020.

Taarifa ya TMA imeitaja mikoa hiyo ni; Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Pwani pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba visiwani Zanzibar.

Imesema athari zinazoweza kujitokeza baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Taarifa hiyo imesema kesho Jumatano Machi 4, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa, Njombe, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Alhamisi ya Machi 5, 2020 mvua hizo zinatarajia kunyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa, Njombe, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Chanzo: mwananchi.co.tz