Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua ipo mapaka Juni - TMA

Mvua Yawatenga Wananchi Wa Kata Ya Maboga Na Wengine Mvua ipo mapaka Juni - TMA

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua zinazonyesha kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya nchi zitaendelea mpaka mwezi wa sita mwaka huu na vitakuwa ni vipindi vifupi na virefu vya mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha madhara ikiwemo mafuriko na magonjwa ya milipuko.

Hivyo ni vyema wananchi wakachukua tahadhari

Akizungumza nasi leo, Mtaalam na Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA Joyce Makwata, amesema mikoa ambayo itaathirika zaidi na mvua hizo ni Ile ya Dar es Salaam Tanga, Pwani, Morogoro, Visiwa vya Unguja na Mafia.

Amesema licha ya kwamba mvua hizo ni za masika lakini wananchi wanapaswa kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu taarifa za mamlaka ili kufahamu mwelekeo wa hali ya hewa kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live