Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua iliyoezua mapaa yasababisha hasara ya Sh15 milioni

10145 Pic+mvua TanzaniaWeb

Sun, 5 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi. Mvua ya upepo iliyonyesha jana  Agosti 3, 2018 katika kijiji cha Iteja Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imesababisha hasara ya zaidi ya Sh15 milioni.

Mvua hiyo imeezua paa za nyumba kadhaa ikiwemo vyumba vya madarasa katika shule  sekondari Aimee Mirembe.

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 4, 2018 mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda amesema paa la madarasa mawili, vyoo vya wanafunzi na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Isuka iliyoko kata ya Kasololo wilayani humo pia yameezuliwa.

"Paa la nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Kwima pia limeezuliwa," amesema Sweda.

Ofisa elimu sekondari Wilaya ya Misungwi, Diana Kubofa amesema hasara iliyosababishwa na mvua hizo ni zaidi ya Sh15 milioni.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama  iliyotembelea  kijiji hicho kukagua madhala ya mvua, mkuu wa shule ya sekondari Aimee Mirembe, Florencia Ndubashe amesema vyumba vinne vya madarasa, ofisi ya walimu pamoja na vyumba viwili vya maabara vimeezuliwa paa.

"Hii ni mara ya pili miundombinu ya majengo katika shule yetu yanaathiriwa na mvua ya upepo. Mwaka 2013 mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliezua paa ya vyumba viwili vya madarasa," amesema Mwalimu Ndubashe.

Mkuu wa wilaya amesema mchakato wa kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa imeanza kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo haraka iwezekanavyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz