Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi atuhumiwa kumbaka Mgonjwa

Muuguzi Abaka Muuguzi atuhumiwa kumbaka Mgonjwa

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muuguzi mmoja wa Hospitali ya Wilata ya Sikonge Mkoa wa Tabora anatuhumiwa kumbaka Binti mmoja (jina limehifadhiwa) Mgonjwa aliyekuwa amelazwa Hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Simon Chacha amesema tukio hilo limetokea usiku wa June 9, 2023 katika Hospitali hiyo wakati Binti huyo alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria na UTI.

Chacha amesema baada ya tukio hilo Serikali imechukua hatua za kinidhamu kwa kumsimamisha kazi Muuguzi huyo na kwamba Polisi wapo katika hatua za mwisho za uchunguzi kabla ya kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live